Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб Live ▶|| Ibada Ya Morning Glory | 04 - 07 - 2024 в хорошем качестве

Live ▶|| Ibada Ya Morning Glory | 04 - 07 - 2024 Трансляция закончилась 1 месяц назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



Live ▶|| Ibada Ya Morning Glory | 04 - 07 - 2024

Karibu katika Ibada ya Masifu ya Asubuhi kutokea hapa kanisa Kuu Azania Front Posta Dar Es Salaam. ▶ SOMO: USIOGOPE VITA SI YAKO, VITA NI YA BWANA NA USHINDI NI HAKI YAKO. ............................. ZABURI 130 1 SAMWELI 4: 1 - 11, 17 - 18 1 [Ikawa siku zile Wafilisti walikusanyika ili kupigana na Israeli,] nao Waisraeli wakatoka juu ya Wafilisti kwenda vitani; wakatua karibu na Ebenezeri, nao Wafilisti wakatua huko Afeki. 2 Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Waisraeli wakapigwa na Wafilisti; waliowaua karibu elfu nne katika uwanja wa vita. 3 Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo hadi huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu. 4 Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la Agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la Agano la Mungu. 5 Na sanduku la Agano la BWANA lilipoingia kambini, Israeli wote wakapiga kelele kwa sauti kuu, hata nchi ikavuma. 6 Nao Wafilisti waliposikia mshindo wa zile kelele, walisema, Maana yake nini mshindo wa kelele hizi kubwa katika kambi ya Waebrania? Wakatambua ya kuwa sanduku la BWANA limefika kambini. 7 Wafilisti wakaogopa, maana walisema, Mungu ameingia kambini. Wakasema, Ole wetu! Kwani halijawa jambo kama hili tangu hapo. 8 Ole wetu! Ni nani anayeweza kutuokoa kutoka kwa miungu hawa wenye nguvu? Hawa ndio miungu waliowapiga Wamisri kwa mapigo ya kila namna jangwani. 9 Jipeni moyo, na kufanya kiume enyi Wafilisti, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama wao walivyokuwa watumwa wenu; fanyeni kiume, mkapigane nao. 10 Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu elfu thelathini walioenda vitani kwa miguu. 11 Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa. 17 Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa. 18 Ikawa alipolitaja sanduku la Mungu, Eli akaanguka kitini pake kwa nyuma, kando ya mlango, shingo yake ikavunjika, akafa; maana alikuwa mzee, tena mzito. Naye alikuwa amewaamua Waisraeli miaka arubaini. 1 SAMWELI 7: 5 - 6 5 Samweli akasema, Wakusanyeni Waisraeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA. 6 Wakakusanyika huko Mispa, wakateka maji na kuyamimina mbele za BWANA; wakafunga siku ile, wakasema huko, Tumemfanyia BWANA dhambi. Samweli akawaamua wana wa Israeli huko Mispa. 1 SAMWELI 5: 1 - 4 1 Basi Wafilisti walikuwa wamelichukua sanduku la Mungu, wakaenda nalo kutoka Ebenezeri hadi Ashdodi. 2 Wafilisti wakalichukua sanduku la Mungu, wakalitia katika nyumba ya Dagoni, wakaliweka karibu na Dagoni. 3 Na watu wa Ashdodi, walipoamka alfajiri siku ya pili, kumbe! Dagoni imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA. Wakaitwaa Dagoni, wakaisimamisha mahali pake tena. 4 Hata walipoamka kesho yake asubuhi, kumbe! Dagoni ilikuwa imeanguka chini kifudifudi, mbele ya sanduku la BWANA; na kichwa chake Dagoni na vitanga vyote viwili vya mikono yake vimekatika, na kulazwa kizingitini; Dagoni ikasalia kiwiliwili chake tu. 1 SAMWELI 6: 1 - 3 1 Basi, hilo sanduku la BWANA lilikuwamo katika nchi ya Wafilisti muda wa miezi saba. 2 Nao Wafilisti wakawaita makuhani na waaguzi, wakasema, Tulifanyieje sanduku la BWANA? Tuonesheni jinsi tuwezavyo kulirudisha mahali pake. 3 Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu. 1 SAMWELI 7: 7 - 10, 12 12 Ndipo Samweli akatwaa jiwe, na kulisimamisha kati ya Mispa na Sheni, akaliita jina lake Ebenezeri, akisema, Hata sasa BWANA ametusaidia. ▶ Mhubiri: Ev. Geofrey Simon Mbwambo ............. 👇👇👇 // NAMBA ZA SADAKA // ▶ LIPA KWA [ M-PESA ] - 579 579 4 ▶ NAMBA YA MPESA - 0757 - 391 - 174 JINA: KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL ▶ MAENDELEO BANK A/C NO 0137 9274 6021 JINA: LUTHERAN CHURCH AZANIA FRONT CATHEDRAL TUFUATILIE KWENYE MITANDAO KWA TAHARIFA ZAIDI: Instagram page: / kkkt_azaniafront_cathedral Website: https://www.azaniafront.org/ Facebook: / kkkt-azania-front-cathedral-101434162039079 #azaniafrontcathedral #ibada #lunchhour #morningglory #sundayservice #lutheran

Comments