Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб Aeleza walichozungumza saa chache kabla ya kutoweka mchumba wake в хорошем качестве

Aeleza walichozungumza saa chache kabla ya kutoweka mchumba wake 2 недели назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



Aeleza walichozungumza saa chache kabla ya kutoweka mchumba wake

Neema Mmasy, mchumba wa muuguzi wa Hospitali ya KCMC, Lenga Masunga (38) aliyetoweka katika mazingira ya kutatanisha ameeleza mara ya mwisho alivyozungumza na mchumba wake huyo akimtaarifu kwamba ametoka kazini. Amesema wamekuwa na utaratibu wa kuwasiliana mara kwa mara wakati wa kwenda kazini na kutoka. Amesema Julai 2, saa 10 jioni aliwasiliana naye na kumtaka aendelee na majukumu yake kwa kuwa wangewasiliana baadaye. Neema amesema ilipofika saa tatu usiku alishangaa kuona amekuwa kimya na hajamtafuta ndipo alimpoamua kumpigia simu na hakupatikana. Hayo ameeleza leo Jumatano, Julai 10 2024, wakati akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu taarifa za kutoonekana kwa mchumba wake huyo. Muuguzi huyo wa idara ya masikio, pua na koo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Julai 2, mwaka huu nyumbani kwake Mtaa wa Rau Pangaleni, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro alikokuwa akiishi.

Comments