Русские видео

Сейчас в тренде

Иностранные видео


Скачать с ютуб Nahodha || Dodoma Adventist Chorus в хорошем качестве

Nahodha || Dodoma Adventist Chorus 2 месяца назад


Если кнопки скачивания не загрузились НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу страницы.
Спасибо за использование сервиса savevideohd.ru



Nahodha || Dodoma Adventist Chorus

NAHODHA Siku moja Yesu aliwaambia Wanafunzi wake hebu na tuvukeni ng'ambo Wakapanda wote ndani ya chombo Mara tufani chombo kikaanza kujaa maji Wakati huo Yesu amelala Wakamwendea kumwamsha "Bwana Twaangamia" Akasimama, kakemea upepo kukawa shwari dhoruba zikakoma Kisha akageuka (Kisha akageuka) Akawauliza (Akawauliza) Imani yenu i wapi (Je imani yenu i wapi nao wakaogopa) Ni nani huyu ambaye (Je ni nani huyu ambaye) Pepo na Bahari vinasikia sauti yake. Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu Mikononi mwake chombo huwa salama. Unawezamwamini maana Chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha Mambo yote huwa salama Katikati ya Dhoruba na Shida Pepo zivumapo na Bahari ichafukapo Unaweza kudhani amelala Na hajali kuhusu shida zote upitiazo "Je ni kweli huyu ndiye ambaye Alisema 'takuwa nami Tena nisiogope Nina mashaka na uwezo wake Je ni kweli anaweza kuokoa?" Usiogope ndugu (Usiogope ndugu) Na usifadhaike (Na usifadhaike) Imani yako weka kwake (hajawahi kushindwa) Nahodha huyu si mwingine Bali Bwana Yesu, amini utafika salama Huyu ni Nahodha.. Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu Mikononi mwake chombo huwa salama. Unawezamwamini maana Chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha Mambo yote huwa salama Mambo huwa ni salama Bwana Yesu akiwa ni Nahodha Huyu ni Nahodha mwenye uzoefu mkuu (Mikononi mwake) Mikononi mwake chombo huwa salama. (Usiwe na shaka) Unawezamwamini maana chombo hakijawahizama Akiwa ni Nahodha (Akiwa ni Nahodha..) Mambo yote huwa salama (Bwana akiwa chomboni) Mambo yote huwa salama (Weka tumaini lako kwake) Mambo yote huwa salama. Luka 8:22-25 [22]Ikawa siku zile mojawapo alipanda chomboni yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke mpaka ng’ambo ya ziwa. Wakatweka matanga. [23]Nao walipokuwa wakienda, alilala usingizi. Ikashuka tufani juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika hatari. [24]Wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana mkubwa, Bwana mkubwa, tunaangamia. Akaamka, akaukemea upepo na msukosuko wa maji, vikakoma; kukawa shwari. [25]Akawaambia, Imani yenu iko wapi? Wakaogopa, wakamaka, wakisema wao kwa wao, Ni nani huyu basi hata anaamuru upepo na maji, navyo vyamtii? Artist: Dodoma Adventist Chorus Song Title: Nahodha Audio Mixing and mastering: Job Music Video: RJ Studio (Mr RJ) Email: [email protected] CONTACTS +255 746 698 570 +255 622 309 142 You can also find us on: https://audiomack.com/dodomaadventist... Instagram   / dodomaadventistchorus   and all other digital platforms for audio.

Comments